Sahara ni jangwa kubwa katika Afrika ya Kaskazini na Afrika ya Magharibi pia ni jangwa kubwa kabisa duniani. Ina eneo la 9,065,000 km² sawa na eneo la Marekani au karibu sawa na eneo lote ya Ulaya. Jina lake ni neno la kiarabu (صحراء sahra' ) linalomaananisha "jangwa".
Wataalamu wa jiografia huamini ya kwamba haikuwepo wakati wote. Kutokana na utafiti wa dalili katika udongo na mawe yake eneo la Sahara katika milenia zilizopita lilikuwa na mfululizo wa vipindi vya ukame na vipindi vya mvua.
Nchi zenye sehemu kubwa ya maeneo yao katika Sahara ni hizi: Misri, Libya, Mali, Niger, Chad, Sudan, Mauretania, Sahara ya Magharibi, Moroko, Algeria und Tunisia.
Kuna milima mikubwa kama milima ya Ahaggar, Tibesti na Aïr. Mlima mrefu ni Emi Koussi (3415 m) kwenye milima ya Tibesti katika Chad.
Mnamo miaka 7000 iliyopita Sahara ilikuwa eneo nusu yabisi penye maji katika mito mirefu. Labda inawezekana kuilinganisha na Kenya ya Kaskazini ya leo. Watu walivinda na kufuga wanyama. Mnamo miaka 5000 iliyopita Sahara ilikauka kufikia hali yabisi kama leo. Lakini maji ya mvua ya nyakati zile bado yapo chini ya ardhi. Misri na Libya ina miradi mikubwa kutumia maji yale kwa pampu na kuanza kilimo jangwani kabisa.
Disierto d'o Sajara | صحراء كبرى | Сахара | Sàhara | Sahara | Sahara | Sahara | Sahara | Sahara | Sahara | Desierto del Sahara | Saharo | Désert du Sahara | An Sahára | Deserto do Sáhara | 사하라 사막 | Sahara | Sahara | Sahara | Deserto del Sahara | מדבר סהרה | Szahara sivatag | Sachara | Sahāras tuksnesis | Сахара | Sahara | サハラ砂漠 | Sahara | Sahara | Deserto do Saara | Deşertul Sahara | Пустыня Сахара | Sahara | Sahara Desert | Sahara | Сахара | Sahara | Sahara | சஹாரா | ทะเลทรายซาฮารา | Sara | 撒哈拉沙漠