| (Details) | (Details) |
Ruanda (kifaransa: Le Rwanda) ni nchi ya Afrika ya Mashariki ikipakana na Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda na Tanzania.
Rwanda imepakana na Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda na Tanzania. Mpaka na Kongo ni hasa ziwa la Kivu ambayo ni ziwa mojawapo la bonde la ufa la Afrika ya Mashariki. Mpakani na Kongo na Uganda ndiyo milima ya kivolkeno ya Virunga penye sokwe wa milimani.
Rwanda huitwa nchi ya vilima elfu, (Kifaransa: Pays de Mille Collines) hivyo ndivyo sehemu kubwa ya eneo lake inavyoonekana hasa katika magharibi.
Kigali ni mji mkuu penye kiwanja cha ndege cha kimataifa na mahoteli makubwa.
Gisenyi ni mji kwenye ncha ya kaskazini ya Ziwa la Kivu mpakani na Kongo ikiwa jirani na mji wa Goma. Kuna usafiri wa mashua kwenda Kibuye na Cyangugu.
Kibuye ni mji mdogo ufukoni wa Ziwa la Kivu. Pana wavuvu wengi, kituo cha watalii na nyumba za kihistoria za wamisionari. Hadi 1994 Watutsi 250,000 waliishi katika wilaya ya Kibuye lakini tangu uangamizaji wa Watutsi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe wamebaki 8000 pekee.
Butare ni kitovu cha kiutamaduni katika kusini ya nchi penye chuo kikuu.
Wakati wa ukoloni Wabelgiji walihesabu mnamo mwaka 1931 wakazi wa nchi kama wafuatavyo: 84 % Wahutu, 15 % Watutsi na 1 % Watwaa. Kabla ya uhuru ilitokea mara kwanza vita vya wenyewe kati ya makabila iliyosababisha kupungua kwa Watutsi kutokana na mauaji na zaidi Watutsi kukimbilia nchi jirani. Mnamo 1990 asilimia ya Watutsi ilikadiriwa kuwa 9 - 10 %.
Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya miaka ya 1990 ilileta uangamizaji wa Watutsi waliouawa kwa wingi. Kati ya asilimia 75% hadi90% ya wakazi Watutsi waliuawa katika wiki chache za mwaka 1994. Baada ya mwisho wa vita Watutsi wengi ambao wenyewe au wazazi wao walikuwa wamekimbilia Uganda na Tanzania walirudi tena Rwanda.
Rwanda ilikuwa ufalme tangu karne ya 16 BK. Mwanzo wa karne ya 20 ilikuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Rwanda ikawa koloni ya Ubelgiji. Uhuru katika mwaka 1961 ilifika pamoja na vity ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Wahutu na Watutsi. Uhusiano kati ya vikundi hivi viwili uliendelea kuwa vigumu. Kuuawa kwa rais Habariyama mwaka 1994 kulisababisha mauaji ya watu kama milioni moja. Kikundi cha RPF chini ya Paul Kagame kilingia kati na kuchukua madaraka.
Rwanda | ሩዋንዳ | Ruanda | رواندا | Руанда | Ruanda | Rwanda | Rwanda | Rwanda | Ruanda | Ρουάντα | Rwanda | Ruando | Ruanda | Rwanda | Ruanda | رواندا | Ruanda | Rwanda | Ruanda - Rwanda | רואנדה | रवांडा | Ruanda | Ruanda | Rwanda | Ruanda | Rúanda | Ruanda | ルワンダ | Rwanda | Rwanda | 르완다 | Rwanda | Ruanda | Ruanda | Ruanda | Руанда | Rwanda | Ruanda | Rwanda | Rwanda | Rwanda | Rwanda | Rwanda | Ruanda | Ruanda | Руанда | Rwanda | Ruanda | Rwanda | Rwanda | Ruanda | Ruanda | Руанда | Rwanda | Rwanda | Ruanda | رۋاندا | Руанда | Rwanda | 卢旺达 | Rwanda