Dahomey ilikuwa jina la jamhuri ya Benin hadi 1975 lakini hasa jina la ufalme wa Afrika ya Magharibi katika eneo la Benin ya kusini ya leo.
Waaja wa Abomey walichanganya na wenyeji wakawa kabila jipya la Wafon au Wadahomey. Waliratibu ufalme wao kwa kuupa serikali ya mfalme mwenye nguvu wakaunda jeshi la kudumu. Hasa mfalme Wegbadja aliweka utaratibu kwa vizazi vilivyofuata: mfalme alikuwa mtawala mkuu, mkoani au majimboni hapana watawala wa kineo bali watumishi wake tu.
Ardhi yote ilitazamiwa kuwa mali ya mfalme mwenyewe, mafundishho yaliyohakikisha malipo ya kodi kutoka kwa wakulima waliokubali ya kwamba nchi waliyoilima ilikuwa mali ya mfalme.
Mamlaka ya mfalme yalihakikisha nguvu ya Dahomey katika mazingira yake. Jeshi la kudumu lilimpatia chombo muhimu. Ndani ya jeshi hili kulikuwako kikosi kimoja cha pekee ambacho kilikuwa kikosi cha wanawake. Wasafiri wa Ulaya walikiita kikosi hiki "Waamazoni" kutokana na askari za kike katika masimulizi ya Wagiriki wa Kale.
Wegbadja na wafuasi wake walikaza pia umuhimu wa ibada za pamoja. Wafalme wenyewe na mizimu yao walipewa nafasi muhimu. Sadaka zilienda na kila nafasi, hasa sadaka kwa mizimu wa wafalme.
Ufalme uliongezeka nguvu ya kiuchumi kutokana na biashara ya watumwa. Kupaa kwa nguvu ya Dahomey kulikwenda sambamba na kuenea kwa wafanyabiashara Wazungu kwenye pwani za Afrika ya Magharibi walionunua watumwa kwa ajili ya safari ya Marekani wakiuza silaha na bidhaa kutoka Ulaya. Katika karne tatu za historia yake Dahomey ilikuwa kati ya wafanyabiashara wakuu wa watumwa. Jeshi la Dahomey lilikuwa na bunduki zilizonunuliwa na Wazungu wakiwauzia watumwa; silaha hizi zilitumika kwa ajili ya vita dhidi ya majirani na kujipatia wafungwa waliouzwa kama watumwa. Mapato kutoka biashara hiyo yaliwezesha wafalme wa Dahomey kununua silaha mpya.
Dahomey | Dahomey (Königreich) | Dahomey | Dahomee | داهومی | Dahomey | דהומיי | Dahomey | Dahómey | ダホメ王国 | Dahomej | Daomé | Dahomey | Dahomey