article

Ardhi au Dunia ni mojawapo ya sayari zinazotembea katika anga ya ulimwengu. Kuna sayari tisa zinazolizunguka jua, ardhi ikiwa sayari ya tatu katika mfumo wa jua na sayari zake. Masafa baina yake na jua ni kilomita milioni 150 au maili milioni 93.2. Ardhi huchukua siku 365.256 kulizunguka jua, na masaa 23.9345 kuuzunguka mhimili wake. Ardhi ina upana wa kilomita 12,756 (maili 7,973) na uzito wa kilogramu 5.97e24

Sura ya dunia au eneo la ardhi yote ni 510,066,000 kilomita mraba, ikiwa nchi kavu imechukuwa eneo la 148,647,000 kilomita mraba na maji yamechukuwa eneo la 361,419,000 kilomita mraba. Eneo la maji kulingana na eneo la nchi kavu ni asilimia 70.9, na nchi kavu 148,647,000 kilomita mraba ni asilimia 29.1.

Kati ya maeneo yaliyofunikwa na maji ni bahari yanayofunika eneo la 335,258,000 kilomita mraba ambalo ni asilimia 97, na maji yaliyobakia matamu ya maziwa, mabwaba na mitoni ni asilimia 3 tu.

Tabaka za ardhi


Ardhi ina tabaka saba ambazo zinahitalifiana kwa ukubwa, na kila moja ina tabia yake.
Tabaka Kuanzia kilomita
Tabaka ya kwanza 0 - 40
Tabaka ya pili 40 - 400
Tabaka ya tatu 400 - 650
Tabaka ya nne 650 - 2700
Tabaka ya tano 2700 - 2890
Tabaka ya sita 2890 - 5150
Tabaka ya saba 5150 - 6370
Kila ukiingia ndani ardhi inazidi kuwa moto mpaka ukifika ndani kabisa daraja ya harara hufikia nyuzi 5000-6000°C.

Hewa ya ardhi


Ardhi ni sayari pekee mpaka sasa ambayo binadamu na viumbe vyengine vya ardhini vinaweza kuishi na hii ni kwa sababu hewa yake ni ya namna ya pekee. Kuna katika hewa ya ardhi asilimia 78 ya naitrojini, asilimia 21 ya oksijini na asilimia 1 ya aina nyenginezo za hewa, na kwa sababu hii uhai na maisha yanamakinika katika ardhi, kinyume na sayari nyenginezo.

Kuumbwa kwa ardhi


Kabla ya kuumbwa kwa ardhi, mbingu zote na ardhi zilikuwa kitu kimoja kilichoambatana kisha Mwenyezi Mungu akavitatanua na kusababisha mlipuko mkubwa kabisa ambao ulitawanya na kupeperusha kila kitu katika anga, na haya yanakubaliana na nadharia ya sayansi leo inayosema kuwa ulimwengu ulianza na mlipuko mkubwa.

Kuhusu ardhi


Sehemu kubwa kabisa ya ardhi inafunikwa na bahari, kwani takriban asilimia 70 ya ardhi inafunikwa na maji ya bahari na kutokana na maji yote yaliyokuwepo ardhini, asilimia 97 ni maji ya bahari, na asilimia 3 ni maji matamu.
Bahari Kuu Eneo lake Kina chake
Pasifiki maili 64,186,000 muraba futi 15,215
Atlantiki maili 33,420,000 muraba futi 12,881
Bahari Hindi maili 28,350,000 muraba futi 13,002
Bahari ya Antaktika maili 7,848,300 muraba futi 13,100 - 16,400
Bahari ya Aktika maili 5,106,000 muraba futi 3,953

Juu ya ardhi


Hewa iliyoko juu ya ardhi vile vile ina tabaka saba, na kila tabaka ina kazi yake. Hewa kwa jumla ina masafa ya kiasi cha kilomita 560 au maili 348 kuendea juu, na baada ya hapo unaingia kwenye anga za juu. Hewa hii ndio inayotukinga sisi viumbe na madhara ya jua na vitu vyenginevyo ambavyo vinaingia anga la dunia na kuteremka ndani ya ardhi.

Sayari

Aarde | Erde | Eorðe | أرض | Tierra | Зямля | Земя (планета) | পৃথিবী | Douar (planedenn) | Zemlja (planeta) | Terra | Země | Zemia | Daear | Jorden | Erde | Γη | Earth | Tero | Tierra | Maa (planeet) | Lurra | زمین | Maa | Terre | Ierde | Terra (planeta) | પૃથ્વી | כדור הארץ | पृथ्वी | Zemlja | Föld | Terra | Bumi | Daga (planeta) | Tero | Jörðin | Terra | 地球 | terdi | დედამიწა | Ntoto | 지구 | Erd | Dor | Terra | Äerd | Eerd | Mabelé | Žemė | Zeme | Земја | Bumi | Art | Cemānāhuac | Eer | Eerde | पृथ्वी | Aarde (planeet) | Jorda | Jorden | Tèrre | Yatu | Ziemia | Terra | Phuv | Pământ | Земля | Terra | The Yird | Zemlja | Earth | Zem | Zemlja | Toka | Земља (планета) | Marcapada | Jorden | பூமி | โลก | Daigdig | Yer (gezegen) | اغايلىماق (ئاسترونومىيە) | Земля (планета) | Trái Đất | 地球 | Tē-kiû | 地球

 

This article is licensed under the GNU Free Documentation License. It uses material from the "Ardhi".

Home Pageartsbusinesscomputersgameshealthhospitalshomekids & teensnewsphysiciansrecreationreferenceregionalscienceshoppingsocietysportsworld