article Related Topics:
Afrikaans :: Afrika_Bambaataa :: Afrikaner :: Afrika :: Afrikaans_and_English :: Afrikaans_Based
 

Afrika ni bara kubwa la pili duniani. Bara hili lina eneo la kilometa za mraba 30,244,050 na zaidi ya wakazi milioni 800. Asia ndio bara pekee kubwa kushinda Afrika.

Jina la Afrika


Neno "Afrika" limepatikana kutokana na lugha ya Kilatini ya Waroma wa Kale. Waroma hawakumaanisha bara lote kwa jina hili bali eneo katika Tunisia ya leo tu. Asili yake ni katika kabila au taifa la "Afrig" walioishi sehemu zile.

Wakati huu Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini ya Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).

Katika ramani za kale kutoka Ulaya maneno yote matatatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara. Jina la "Afrika" limekuwa kawaida kuanzia karne ya 16. BK.

Lugha


tazama makala "Lugha za Afrika"

Zaidi ya lugha elfu ya Kiafrika zinazungumzwa katika Afrika leo. Lugha za Ulaya zinazumgumzwa pia, haswa Kiingereza, Kifaransa na Kireno. Kiafrikaans ni lugha ya pekee ya Afrika Kusini yenye asili ya Ulaya. Lugha za Kibantu (kwa mfano Kiswahili) ni lugha muhimu katika Afrika ya Kusini, Afrika ya Kati na Afrika ya Mashariki. Kiarabu ni lugha muhimu Afrika ya Kazakazini.

Orodha ya nchi na maeneo kufuatana na kanda za bara (1)


Afrika ya Mashariki:

BurundiKomoroJibutiEritreaEthiopiaKenyaMadagaskaMalawiMauritiusMayotte (Ufaransa) MsumbijiRéunion (Ufaransa) RwandaShelisheliSomaliaSudanTanzaniaUgandaZambiaZimbabwe
Jina la nchi au eneo,
bendera
Eneo
(km²)
Wakazi
(mnamo Julai 2002 takriban)
Wakazi kwa km² Mji Mkuu
27,830 6,373,002 229.0 Bujumbura
2,170 614,382 283.1 Moroni
23,000 472,810 20.6 Djibouti
121,320 4,465,651 36.8 Asmara
1,127,127 67,673,031 60.0 Addis Ababa
582,650 31,138,735 53.4 Nairobi
587,040 16,473,477 28.1 Antananarivo
118,480 10,701,824 90.3 Lilongwe
2,040 1,200,206 588.3 Port Louis
374 170,879 456.9 Mamoudzou
801,590 19,607,519 24.5 Maputo
2,512 743,981 296.2 Saint-Denis
26,338 7,398,074 280.9 Kigali
455 80,098 176.0 Victoria
637,657 7,753,310 12.2 Mogadishu
2,505,810 37,090,298 14.8 Khartoum
945,087 37,187,939 39.3 Dodoma
236,040 24,699,073 104.6 Kampala
752,614 9,959,037 13.2 Lusaka
390,580 11,376,676 29.1 Harare

Afrika ya Kati

AngolaKamerunJamhuri ya Afrika ya KatiChadiKongo, Jamhuri yaKongo, Jamhuri ya KidemokrasiaGuinea ya IkwetaGabonSão Tomé na Príncipe
Jina la nchi au eneo,
bendera
Eneo
(km²)
Wakazi
(mnamo Julai 2002 takriban)
Wakazi kwa km² Mji Mkuu
1,246,700 10,593,171 8.5 Luanda
475,440 16,184,748 34.0 Yaoundé
622,984 3,642,739 5.8 Bangui
1,284,000 8,997,237 7.0 N'Djamena
342,000 2,958,448 8.7 Brazzaville
2,345,410 55,225,478 23.5 Kinshasa
28,051 498,144 17.8 Malabo
267,667 1,233,353 4.6 Libreville
1,001 170,372 170.2 São Tomé

Afrika ya Kaskazini

AlgeriaMisri (2) LibyaMoroko

TunisiaVisiwa vya Kanari(Hispania) (3) Ceuta (Hispania) (4) Visiwa vya Madeira (Ureno)(5) Melilla (Hispania) (6)
Jina la nchi au eneo,
bendera
Eneo
(km²)
Wakazi
(mnamo Julai 2002 takriban)
Wakazi kwa km² Mji Mkuu
2,381,740 32,277,942 13.6 Algiers
1,001,450 70,712,345 70.6 Cairo
1,759,540 5,368,585 3.1 Tripoli
446,550 31,167,783 69.8 Rabat
163,610 9,815,644 60.0 Tunis
Maeneo ya Hispania na Ureno katika Afrika ya Kaskazini:
7,492 1,694,477 226.2 Las Palmas de Gran Canaria,
Santa Cruz de Tenerife
20 71,505 3,575.2
797 245,000 307.4 Funchal
12 66,411 5,534.2

Afrika ya Kusini

BotswanaLesothoNamibiaAfrika Kusini (7) Uswazi
Jina la nchi au eneo,
bendera
Eneo
(km²)
Wakazi
(mnamo Julai 2002 takriban)
Wakazi kwa km² Mji Mkuu
600,370 1,591,232 2.7 Gaborone
30,355 2,207,954 72.7 Maseru
825,418 1,820,916 2.2 Windhoek
1,219,912 43,647,658 35.8 Bloemfontein, Cape Town, Pretoria
17,363 1,123,605 64.7 Mbabane

Afrika ya Magharibi

BeninBurkina FasoCabo VerdeCôte d'Ivoire (8) GambiaGhanaGuineaGuinea-BissauLiberiaMaliMauritaniaNigerNigeriaSaint Helena (Uingereza) SenegalSierra LeoneTogoSahara ya Magharibi (Moroko) (9)
Jina la nchi au eneo,
bendera
Eneo
(km²)
Wakazi
(mnamo Julai 2002 takriban)
Wakazi kwa km² Mji Mkuu
112,620 6,787,625 60.3 Porto-Novo
274,200 12,603,185 46.0 Ouagadougou
4,033 408,760 101.4 Praia
322,460 16,804,784 52.1 Abidjan, Yamoussoukro
11,300 1,455,842 128.8 Banjul
239,460 20,244,154 84.5 Accra
245,857 7,775,065 31.6 Conakry
36,120 1,345,479 37.3 Bissau
111,370 3,288,198 29.5 Monrovia
1,240,000 11,340,480 9.1 Bamako
1,030,700 2,828,858 2.7 Nouakchott
1,267,000 10,639,744 8.4 Niamey
923,768 129,934,911 140.7 Abuja
410 7,317 17.8 Jamestown
196,190 10,589,571 54.0 Dakar
71,740 5,614,743 78.3 Freetown
56,785 5,285,501 93.1 Lomé
266,000 256,177 1.0 El Aaiún
Total 30,368,609 843,705,143 27.8

Maelezo:

  1. Kanda zinazotajwa (Afrika ya Kusini – Magharibi n.k.) zinafuata utaratibu wa Umoja wa Mataifa United Nations geographical subregions.png.
  2. Misri imo Afrika lakini sehemu ya eneo lake iko Asia ya Magharibi. Wengine huiita nchi ya kimabara.
  3. Visiwa vya Kanari ni sehemu ya Hispania ikiwa Las Palmas de Gran Canaria pamoja na Santa Cruz de Tenerife ndiyo miji mikuu pamoja mara nyingi huhesabiwa kuwa sehemu ya Afrika ya Kaskazini; viko karibu na Moroko and Sahara ya Magharibi; wakazi na eneo vya 2001.
  4. Mji wa Ceuta ni eneo la Hispania ufukoni wa Bahari ya Mediteraneo ikizungukwa na nchi ya Moroko; wakazi na eneo ni ya 2001.
  5. Visiwa vya Madeira ni sehemu ya Ureno, mara nyingi huhesabiwa kuwa sehemu ya Afrika ya Kaskazini viko karibu na Moroko; wakazi na eneo vya 2001.
  6. Mji wa Melilla ni eneo la Hispania ufukoni wa Bahari ya Mediteraneo ikizungukwa na nchi ya Moroko; wakazi na eneo ni ya 2001.
  7. Bloemfontein ndiyo makao ya Mahakama Kuu ya Afrika Kusini, Cape Town ni makao ya Bunge, Pretoria ni makao makuu ya serikali.
  8. Yamoussoukro ndiyo rasmi Mji Mkuu wa Côte d'Ivoire lakini Abidjan ni makao ya serikali hali halisi.
  9. Sahara ya Magharibi imetekwa na kutawaliwa kwa sehemu kubwa na Moroko hali isiyokubalika na jumuiya ya kimataifa .

Afrika | Bara

Afrika | አፍሪቃ | Africa | Africa | أفريقيا | África | Afrika | Африка | আফ্রিকা | Afrika | Afrika | Àfrica | Afrika | Affrica | Afrika | Afrika | Αφρική | Africa | Afriko | África | Aafrika | Afrika | آفریقا | Afrikka | Afrika | Afrique | Africa | Afrika | An Afraic | Afraga | África | આફ્રિકા | אפריקה | Afrika | Afrik | Afrika | Africa | Afrika | Afrika | Afríka | Africa | アフリカ | Afrika | Afrika | ಆಫ್ರಿಕ | 아프리카 | Efrîqa | Afrika | Africa | Afrika | Afrika | Afrika | Āfrika | Afrika | Африка | Afrika | Afrika | Afrika | Afrika | Afrika | Afrika | Afrique | Afryka | África | Africa | Африка | अफ्रीका | Àfrica | Afrihkká | Afrika | Africa | Afrika | Afrika | Aferika | Afrika | Afrika | Африка | Afrika | ஆப்பிரிக்கா | ทวีปแอฟริกา | Afrika | Aprika | Aferika | Afrika | Африка | Châu Phi | אפריקע | 非洲 | Hui-chiu | 非洲

 

This article is licensed under the GNU Free Documentation License. It uses material from the "Afrika".

Home Pageartsbusinesscomputersgameshealthhospitalshomekids & teensnewsphysiciansrecreationreferenceregionalscienceshoppingsocietysportsworld